Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, anasema hata JPM akimteuwa kuwa kiongozi ndani ya serikali ya ccm hatokubali maana ni kinyume na matakwa ya wana ACT kwakua yupo ili aikosowe na hatimae kushika uongozi kwa njia ya kuiondowa ccm madarakani.viongozi wawili tayali wameshatoka katika chama hiki cha ACT na hivyo kuonesha nia ya JPM kuteua kiongozi anaemtaka kutoka chama chote.
viongozi hawa ambao waliasi chama cha ACT wazalendo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira. Viongozi hawa wawili walionesha mfano wa kumtii Rais ila kukisababishia chama kupoteza viongozi wakubwa.
Mbunge huyu aliyasema haya wakati akihojiwa na moja kati ya magazeti maalufu nchini Tanzania. Zitto bado ni Mbunge anaeaminika Kigoma na akiwa na wafuwasi wengi. Katika maneno aliyoyasema kuthibitisha kuwa amegomakuteuliwa na Raisi ni hii: "Sitakubali uteuzi kwa sababu
jukumu langu na viongozi wengine wa ACT Wazalendo ni kujenga chama ili kupata ushawishi na kuungwa mkono na umma na hatimaye kushika dola".
Zitto Kabwe anaamini kuwa kuteuliwa na kukubali uteuzi wowote ndani ya uongozi wa chama tawala ni kufifisha matumaini ya watu walio wengi wanaofuata dila ya chama cha ACT. Kiongozi huyu alipoulizwa kuhusu uteuzi wa viongozi waliotoka chama chake yeye alijibu kuwa wengine walikuwa watumishi wa umma hivyo kabla na baada ya uteuzi wao hakuna kilichobadilika isipokuwa jina au Title ya viongozi hao.
Zitto Kabwe hakatai uteuzi wawanachama wengine ila yeye tu maana anaamini kila mmoja ana
jinsi anavyoelewa siasa anayoifanya na mwelekeo wake.