Baada ya kutangaza mshindi wa uchaguzi nchini kenya, pande moja ambayo ni ya upizani ikiundwa na mkusanyiko wa vyama vya upinzani ( NASA) haijakubaliana na uchaguzi.
siku moja baada ya kutangaza Raisi, Laila Odinga alitangaza kuwa kura zimeibiwa hivyo kuamua kutangaza kuwa kila mwanchi anaekubali mawazo ya uoinzani wakiwemo na polisi wangechukua siku moja bila kwenda kazini kama sehemu ya kuonesha ulimwengu kwamba hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo.
Sambamba na hali hii, kiongozi huyu wa upinzani ametowa kauli kubwa ikiendelea kusisitiza kutokubaliana na matokeo hayo na kuwaomba wanchi wasikubaliane na rais alietangazwa maana wao wanamini walishinda uchaguzi na zikafanyika njia nyingi za kuiba kura. Kilammoja anajuwa kabisa kuwa kabla ya uchaguzi kiongozi wa mitandao ya kitechnologia aliokua na software ya kuhakiki kura aliuliwa na watu ambao hawakujulikana. Hili balaa lilimkuta baada ya kutangaza kua hiyo software hakuna mtu wa kuweza kuiingia wala kuihack bali yeye peke yake.
Wakenya kwasasa wamekaa na kusubili nini kitatokea eitha Laila akubali kua alishindwa au kuamua kivingine. Papohapo Rais Uhuru yeye tayali ameshaanza kutowa onyo na ushauli kwa viongozi wa upinzani kwa kuwataka waandamane na kugomea matokeo ya uchaguzi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi.