Team bora za mpira wa miguu Tanzania zipo na zinafanya vizuri hapahapa nchini na nje ya Tanzania. katika mchezo huu wa mpira wa miguu, Tanzania kama nchi nyingine kuna vikundi namashindano mengi. Ligi kuu ya tanzania hujumuisha team zaidi ya kumi ijapokuwa zinazovuma ni chache.
Hadi sasa inajulikana wazi kuwa mtu anapoongelea soccer ya Tanzania huwa team kubwa mbili ndizo zinazotiliwa maanane na huwa zina mashabiki kuliko team zingine.
Team hizi ni SIMBA na YANGA ambazo zinajinyakulia mashabiki kila kukicha hivyo kuwa wapinzani wakubwa nchini Tanzania.
Kila kukiwa na Mechi inayozihusisha team hizi mbili huwa kila mtu na hata asiependa mpira anatambuwa kuwa kuna mechi siku hiyo. Hii hali husababishwa na mwitikio zikiwemwo na mbwembwe nyingi zinazofanywa na mashabiki wa hizi team.
Ukitupilia mbali uhalibifu wa viti na vitu vingine vilivyopo uwanjani, watu huwa wanaitikia na kujaza uwanja wa mpira wa miguu mkubwa uliopo jijini Dar es salaam.
Team hizi mbili hazichezi zikiwa zenyewetu! AZAM, KAGERA SUGAR, MAJIMAJI, RUVU, MTIBWA na zingine zikiwemo na za kipolisi ndizo zinazoshiliki mashindano na hatimae kupatikana mshindi wa kila mwaka na hasa mambo hunoga zaidi pale Inapofika wakati wa kushindania ngao ya
hisani. hapa ndipo kila mmoja anataka kuonesha ubabe na umahili katika soccer hili la Tanzania.