Roma ni msanii anaehusika sana na kuimba nyimbo au songs za HIP HOP. Katika mashari yake amekuwa akiongelea maswala mengi ya kijamii na ukombozi wa mtu mnyonge. Aliandika nyimbo nyingi zikiwemo nyimbo za kuwakosoa viongozi wa kisiasa na viongozi wa dini. yapo mengi sana yaliowavutia watanzania hadi watu wa nje na Tanzania. nyimbo nyingi zilivuma kote ulimwenguni na hasahasa wimbo wake wa VIVA ROMA.
Sikuchache kabla ya kutoa wimbo wake mpya "Zimbabwe" alitekwa na watu ambao hawakujulikana. katika wimbo wake huu mpya anaongelea ni jinsigani alivyotekwa na kuteswa kwa siku tatu 3 akiwa amefungwa mikono nyuma. anasema alipigwa fimbo ambazo anaziita mijeredi na tena anasema kuwa waliomteka hawakuja na gari ya aina ya noa kama ilivyokua ikisemekana.
Ndani ya wimbo huu anaendelea kuweka wazi kuwa ataendelea kuutetea ukweli na haki inayopatikana katika kitabu kitakatifu "BIBLE" hivyo kuonesha msisitizo juu ya imani yake na Mungu wake. anasema pia kuwa Wote waliomteka na yeye wameumbwa na Mungu mmoja hivyo kuonesha kuwa mbali na vyeo vya duniani wote ni sawa.
Roma huyu anajiuliza maswali katika wimbo huo kuhusu mabadiliko ya uongozi. anasema kua ipo siku moja mpinzani nae atakua Mtawala. anaendelea na anasisitiza kuwa kuwa mpinzani sio dhambi. na analinganisha hali yaupinzani na simba na yanga. anasema yeye ni simba wewe ni yanga, hivyo basi wote ni mashabiki wa mpira mmoja.